1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin atafuta ushirikiano zaidi wa nishati na China

17 Mei 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin leo amejitolea kupanua usambazaji wa nishati kwa China alipokuwa akikaribia mwisho wa ziara yake ya siku mbili nchini humo.

https://p.dw.com/p/4g0hH
China | Urusi
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi JinpingPicha: Sergei Bobylyov/AFP/Getty Images

Rais wa Urusi Vladimir Putin leo amejitolea kupanua usambazaji wa nishati kwa China alipokuwa akikaribia mwisho wa ziara yake ya siku mbili nchini humo.

Akihutubia maonyesho ya biashara ya Urusi na China katika mji wa Harbin, Putin amesema:

"Muungano wetu wa kimkakati katika sekta ya nishati, umekuwa ndio nguzo muhimu katika rasilmali kwenye soko la nishati duniani, nina hakika tutaendelea kuimarika. Urusi iko tayari kusambaza nishati ya uhakika katika uchumi wa China, kwenye sehemu za biashara na katika miji na pia ina uwezo wa kusambaza nishati safi isiyochafua mazingira na kwa bei nafuu.

Ziara ya Putin nchini China, inatazamwa vipi na wajuzi?

Katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa muhula wake wa tano madarakani mapema mwezi huu, Putin amesema ana uhakika ushirikiano wa kimkakati katika sekta ya nishati utaimarishwa zaidi.

Urusi imekuwa chini ya shinikizo la kiuchumi la kutafuta masoko mapya kwa rasilimali zake za nishati tangu uvamizi wake nchini Ukraine mnamo mwaka 2022 kusababisha vikwazo vya Magharibi kwa sekta yake ya mafuta na gesi