Polisi Ujerumani yawatia mbaroni washukiwa wa ugaidi | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Polisi Ujerumani yawatia mbaroni washukiwa wa ugaidi

Polisi nchini Ujerumani imewakamata watu watatu wakihusishwa na  kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu. Ni katika harakati zinazoendelea kuwagundua wanaopanga njama za kufanya mashambulio.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa washukiwa hao walikuwa wanapanga shambulizi kubwa la kigaidi.  Aidha polisi walivamia msikiti mmoja ulioko katika eneo la  Moabit mjini Berlin ambako watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwa mazungumzo. Watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Desemba 19 mwaka jana  katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na raia mmoja wa Tunisia Anis Amri  baada ya kuendesha lori katika soko la Krismasi mjini Berlin lililokuwa limefurika watu hali iliyopelekea serikali ya Ujerumani kuchukua hatua za kuimarisha usalama.

Mwandishi: Isaac Gamba/dw

Mhariri: Gakuba Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com