1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pentagon: Hakuna adhabu kufuatia shambulizi la Kabul

John Juma
14 Desemba 2021

Makao makuu ya kijeshi ya Marekani Pentagon imesema hakuna mwanajeshi yeyote atakayeadhibiwa kufuatia shambulizi la kimakosa lililowaua watu wa familia moja Kabul Afghanistan.

https://p.dw.com/p/44FoV
USA Pentagon-Sprecher John Kirby
Picha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Manusura wa mashambulizi yaliyofanywa kimakosa na Marekani na kuwaua watu 10 wa familia moja kwa kutumia ndege isiyohitaji rubani, wamesema wamesikitishwa na hali kwamba maafisa wa Marekani waliohusika kwenye shambulizi hilo hawatachukuliwa hatua ya kinidhamu.

Zemerai Ahmadi pamoja na ndugu zake wengine watatu ambao ni manusura wa shambulizi hilo lililowaua jamaa wao saba kwa wakati mmoja.

Taliban yaiandikia Marekani barua ya wazi kuihimza kuondoa vikwazo

Akiwa ameketi kando ya barabara hatua chache tu kutoka eneo ambalo makombora ya Marekani yalishambulia gari la kaka yake mnamo Agosti 29 Zemerai amelielezea shirika la habari la Associated Press masikitiko yake.

Wito wa kutaka wahamishwe kutoka Afghanistan haijaitikiwa

Wahanga wa shambulio hilo wanasema hadi leo hawajapata taarifa yoyote kutoka Washington kuhusu fidia au ni linii watahamishwa kutoka Afghanistan.
Wahanga wa shambulio hilo wanasema hadi leo hawajapata taarifa yoyote kutoka Washington kuhusu fidia au ni linii watahamishwa kutoka Afghanistan.Picha: Rahmat GulAP/picture alliance

Ahmadi aliyekuwa na umri wa miaka 37 alikuwa mwajiriwa wa kudumu wa shirika la kiutu la Marekani. Shambulizi lililomuua pamoja na wengine tisa lilifanyika katika siku za mwisho zilizojaa hofu za vikosi vya Marekani kujiondoa Afghanistan kufuatia kundi la Taliban kuchukua udhibiti wa nchi hiyo katikati ya mwezi Agosti.

Marekani yakubali kuisaidia Afghanistan

Shambulizi hilo lilifanyika siku chache tu baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga kufanya shambulio na kuwaua wanajeshi 13 wa Marekani na Waafghani 169 katika uwanja wa ndege mjini Kabul.

Tangu shambulio hilo, familia ya Ahmadi imekuwa ikitaka waliohusika waadhibiwe na wao pia wahamishwe hadi Marekani au taifa jingine ambalo watahisi wako salama.

Siku ya Jumatatu, makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon ilisema waziri wa Ulinzi Lloyd Austin aliyadhinisha mapendekezo ya kuimarisha operesheni zao za mashambulizi miongoni mwa majenerali wanaoongoza kamandi kuu ya Marekani na vilvile kamandi ya operesheni maalum, kulingana na tathmini huru ya Pentagon iliyotolewa mwezi uliopita.

Vikosi vya Marekani viliamini kwamba gari walilokuwa wakilifuatilia lilikuwa kitisho kikubwa hivyo, viliamua kulishambulia.
Vikosi vya Marekani viliamini kwamba gari walilokuwa wakilifuatilia lilikuwa kitisho kikubwa hivyo, viliamua kulishambulia.Picha: Sarahbeth Maney/AP/picture alliance

Msemaji wa Pentagon John Kirby amesema kando na hayo, hakukuwa na mapendekezo ya yaliyotolewa na majenerali kutaka adhabu ichukuliwe.

Marekani,Taliban kufanya mazungumzo ana kwa ana mjini Doha

Kirby aliongeza kwamba Marekani bado iko tayari kuwafidia familia ya Ahmadi kifedha na ikiwezekana iwaondoe Afghanistan. Lakini alipoulizwa ni kwa nini hatua hiyo inachukua muda mrefu, alijibu kwa kusema Marekani inataka ifanye hivyo kwa njia salama zaidi iwezekanavyo.

Vitisho kwa familia ya Ahmadi

Kwa Ahmadi, kuishi Kabul kila siku huwatia katika hatari kubwa. Huwa wanapokea vitisho kupitia simu. Amesema Emal ambaye ni kitinda mimba miongoni mwa vijana hao amesema wanaowapigia simu huwatishia kuwaua ikiwa hawatawapa fedha ambazo wanafikiri Marekani imeshawalipa kama fidia.

"Mara kwa mara watu hutuuliza kiasi cha pesa ambacho Marekani imetulipa, ilhali ukweli ni kwamba tungali tunasubiri. Hatuna chochote. Kadri tunavyosubiri ndivyo hali inazidi kuwa ya hatari kwetu,” amesema Emal.

Wakati wa shambulizi hilo, Marekani ilikuwa ikipanga kuwahamisha maelfu ya Wamarekani waliokuwemo Afghanistan Pamoja na washirika wao, hasa baada ya iliyokuwa serikali ya Afghanistan kuanguka.
Wakati wa shambulizi hilo, Marekani ilikuwa ikipanga kuwahamisha maelfu ya Wamarekani waliokuwemo Afghanistan Pamoja na washirika wao, hasa baada ya iliyokuwa serikali ya Afghanistan kuanguka.Picha: AFP/Getty Images

Waathiriwa wataka wanajeshi wa Marekani waliohusika waadhibiwe.

Kwa Romal Ahmadi ambaye Watoto wake Watoto wenye umri wa kati ya miaka 2-7 waliuawa kwenye shambulizi hilo, kila kunapokucha Maisha yake ni ya huzuni na msongo wa mawazo. Anataka wanajeshi wa Marekani waliohusika waadhibiwe.

"Marekani ni dola lenye nguvu zaidi ulimwenguni. Ilhali sisi hatuna nguvu ya kufanya chochote. Kwa hivyo tunamuachia Mungu awaadhibu,” amesema Romal.

Kwa wiki kadhaa licha ya uwepo wa ushahidi kwamba Marekani iliwaua watu 10 wa familia ya Ahmadi kimakosa, Pentagon ilishikilia kwamba ilimuua mwanachama wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Hadi katikati ya mwezi Septemba ndipo jenerali wa Marekani Frank McKenzie anayeongoza kamandi kuu ya Marekani Afghanistan alikiri kwamba shambulizi hilo lilikuwa kosa kubwa na kusema raia wasiokuwa na hatia waliuawa.

(APE)