Papa Leo asali katika eneo la mlipuko uliouwa zaidi ya watu
2 Desemba 2025
Papa Leo ameitembelea hospitali moja ya wagonjwa wenye matatizo ya kisaikolojia na baadae kusali katika eneo kulikotokea mlipuko mkubwa mwaka 2020 huko Beirut.
Eneo hilo limekuwa kama ishara ya hali na uongozi mbaya wa taifa hilo. Papa Leo alifanya sala ya kimya katika eneo hilo, kisha kukutana na ndugu na jamaa wa watu 218 waliouwawa kwenye mlipuko huo, waliokuwa wamebeba picha za wapendwa wao, wakiwa wamesimama kwenye bohari la mwisho lililosalia na mirundo ya magari yaliyoteketea katika mkasa huo.
Ripoti zinaarifu kuwa miaka mitano baadae, familia hizo zingali zinatafuta haki, kwani hakuna afisa aliyefunguliwa mashtaka kufikia sasa, na kila juhudi za kuanzisha mashtaka zinazuiwa.
Kiongozi huyo wa kidini alikuwa anataka kupeleka ujumbe wa amani Lebanon, taifa linalokabiliana na miaka kadhaa ya migogoro ya kiuchumi na kisiasa.