1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nikki Haley apata ushindi wa kwanza kura za mchujo

Zainab Aziz
4 Machi 2024

Nikki Haley amepata ushindi wake wa kwanza katika kinyang`anyiro cha kugombea nafasi ya kukiwakilisha chama cha Republican.

https://p.dw.com/p/4d8Pu
Marekani | Nikki Haley
Nikki Haley ameshinda jimbo lake la kwanza katika uchaguzi wa mchujo wa RepublicanPicha: Scott Eisen/Getty Images

Nikki Haley amepata ushindi wake wa kwanza katika kinyang`anyiro cha kugombea nafasi ya kukiwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mnamo mwezi wa Novemba nchini Marekani.

Katika uchaguzi huo wa mchujo ndani ya chama cha Republican, Haley alimshinda rais wa zamani, Donald Trump, kwenye jimbo la Washington DC.

Soma pia: Haley bado hajakata tamaa licha ya kushindwa na Trump katika jimbo la South Carolina

Nikki Haley alipata asilimia 62.9 ya kura wakati Trump aliambulia asilimia 33.2.

Hata hivyo, ushindi wa Haley katika jimbo hilo hautabadilisha mwelekeo wa jumla kwani Trump tayari anaongoza kwa kushinda majimbo manane ya awali kwa tafauti kubwa ya kura.