1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Haley aapa kusalia katika kinyang'anyiro licha ya kushindwa

26 Februari 2024

Mgombea urais anayewania uteuzi wa chama cha Republican Nikki Haley amesema bado hajakata tamaa licha ya mpinzani wake Donald Trump kumshinda katika kura za mchujo katika jimbo lake la nyumbani la South Carolina.

https://p.dw.com/p/4csE1
Mgombea urais anayewania uteuzi wa chama cha Republican Nikki Haley
Mgombea urais anayewania uteuzi wa chama cha Republican Nikki HaleyPicha: Brian Snyder/REUTERS

Haley aliyekaidi miito ya kuondoka kwenye kinyang'anyiro hicho, amesafiri kuelekea jimbo la Michigan ambalo litaanda kura zake za mchujo siku ya Jumanne. 

Chini ya saa 24 baada ya kushindwa katika kura za mchujo katika jimbo la South Carolina, timu ya kampeni ya Nikki Haley imesema mgombea huyo amechangisha dola milioni 1 kutoka kwa wafuasi wake mashinani.

Timu hiyo ya kampeni imeeleza kuwa, mchango huo unaonyesha kuwa bado Halley anaungwa mkono na Wamarekani wengi.

Hata hivyo, kundi la kihafidhina lenye nguvu la "Americans For Prosperity Action" limeondoa ufadhili wake katika kampeni ya Nikki Haley.