1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nikki Haley ashinda kura ya mchujo Washington D.C

4 Machi 2024

Mwanasiasa anayewania tiketi ya kuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani, Nikki Haley, ameshinda kura ya mchujo katika wilaya inayojumuisha mji mkuu ya, Washington D.C.

https://p.dw.com/p/4d7rB
Nikki Haley
Nikki HaleyPicha: Brian Snyder/REUTERS

Huo ukiwa ni ushindi wake wa kwanza tangu alipozindua kampeni yake.

Shirika la Habari la Associated Press limeripoti ushindi wa Haley baada ya chama cha Republican kwenye wilaya hiyo kutangaza matokeo rasmi.

Hadi sasa huo ndiyo ushindi pekee alioupata mwanasiasa huyo ambaye anachuana na rais wa zamani Donald Trump kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Republican.

Tangu kuanza kwa kura za mchujo Trump ametangazwa mshindi kwenye majimbo yote yaliyokwishafanya uchaguzi huo wa awali.

Vilevile anatarajiwa kusomba kura zaidi baadaye wiki hii katika siku inayofahamika kama "Jumanne Kuu" ambapo majimbo mengi ya Marekani yanaendesha kura za mchujo.