1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaonya kauli za kuvuruga umoja wake

Sudi Mnette
12 Februari 2024

Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens Stoltenberg jana Jumapili ametoa onyo dhidi ya mazungumzo ambayo "yanadhoofisha usalama" wa jumuiya hiyo.

https://p.dw.com/p/4cHFj
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akiwa katika ofisi za Spika wa Bunge la Marekani.Picha: picture alliance/Bill Clark/CQ Roll Call/Sipa USA

Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens Stoltenberg jana Jumapili ametoa onyo dhidi ya mazungumzo ambayo "yanadhoofisha usalama" baada ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutishia kuhimiza Urusi kushambulia wanachama wa NATO ambao hawajalipa kikamilifu mchango wao kwa jumuiya hiyo.Katika taarifa yake, Stoltenberg amenukuliwa akisema mapendekezo yoyote kwamba washirika hawatalindana yanadhoofisha usalama wao wote, pamoja na ule wa Marekani. Rais huyo wa zamani wa Marekani mara kadhaaamekuwa akikosoa washirika NATO kwa kutoshiriki vyema michango ya operesheni za jumuiya hiyo.