NAIROBI : Somalia yahimniza vikosi vya kulinda amani | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI : Somalia yahimniza vikosi vya kulinda amani

Rais Abdulahi Yusuf Ahmed wa Somalia ametowa wito wa kuwekwa haraka kwa vikosi vya kulinda amani nchini mwake.

Yusuf alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa kundi la mawasiliano la kimataifa kwa ajili ya Somalia uliohudhuriwa na wanadiplomasia wa Kiafrika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi hapo jana.Sehemu kubwa ya wanajeshi hao wa kulinda amani inatazamiwa kuundwa na wanajehi wa Afrika.

Hadi sasa ni Uganda tu iliosema iko tayari kutuma wanajeshi wake nchini Somalia. Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema mjini Kampala hapo jana kwamba kikosi cha Afrika cha kulinda amani nchini Somalia kitafanikiwa kwa sababu Waafrika wanaufahamu mzozo huo vizuri zaidi kuliko wanajeshi wa Marekani waliovyafanya wakati wa shughuli zao zilizopelekea maafa hapo mwaka 1993 nchini humo.

Wakati huo huo ujumbe uliotumwa kwenye mtandao mtu anayeaminika kuwa naibu kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al Zawahiri ametowa wito kwa wapiganaji wa Kiislam kuelekea Somalia na kuendesha mapigano ya chini kwa chini kwa mtindo ule unaotumika Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com