1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanasiasa wa Berlin ashambuliwa katika maktaba

8 Mei 2024

Waziri wa jimbo la Berlin anayeshughulikia masuala ya uchumi, nishati na biashara Franziska Giffey wa chama cha Social Democratic Party, SPD, amejeruhiwa baada ya kushambuliwa katika maktaba katika mji huo mkuu.

https://p.dw.com/p/4fcEu
Franziska Giffey
Meya huyo wa zamani wa Berlin alilazimika kwenda hospitali kutokana na maumivu ya kichwa na shingo.Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Polisi imesema kuwa, mtu mmoja alimshambulia mwanasiasa huyo ghafla kwa kumpiga kwa begi kichwani na shingoni jana mchana.

Soma pia: Matukio ya kushambuliwa wanasiasa nchini Ujerumani kuelekea uchaguzi wa bunge la Ulaya, yaibuwa mshtuko.

Polisi na ofisi ya mwendesha mashtaka ya Berlin wameeleza kuwa meya huyo wa zamani wa Berlin alilazimika kwenda hospitalini kutokana na maumivu ya kichwa na shingo.

Soma pia: Chama cha SPD Berlin chagawika kuhusu muungano na wahafidhina

Na katika tukio jengine, mwanasiasa wa Chama cha Kijani mwenye umri wa miaka 47, Matthias Ecke, pia alitishiwa maisha na kutemewa mate alipokuwa akiweka mabango ya kampeni katika mji wa mashariki wa Dresden.

Polisi inawashikilia watu wawili, wote raia wa Ujerumani, wakiwatuhumu kuhusika na mashambulizi hayo.