1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msumbiji: Ugaidi waongezeka katika jimbo la Cabo Delgado

Zainab Aziz Mhariri:Josephat Charo
14 Agosti 2020

Hali ya usalama kaskazini mwa Msumbiji inazidi kuwa mbaya. Katika siku za hivi karibuni, wapiganaji wenye itikadi kali waliiteka bandari katika eneo hilo la Bahari ya Hindi.

https://p.dw.com/p/3gxTp
Mosambik Fughafen in der Stadt Mocímboa da Praia
Picha: DW/D. Anacleto

Vikosi vya usalama vya Msumbiji hapo jana Alhamisi vilipambana na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislam ili kurudisha tena udhibiti wa bandari muhimu katika jimbo lenye utajiri wa gesi kaskazini mwa Msumbiji. Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Jaime Neto ameeleza hayo leo hii ikiwa ni siku moja baada ya bandari katika mji wa Mocimboa da Praia kutekwa na wapigananaji wenye itikadi kali mapema asubuhi jana.

Wanamgambo hao pia wanasemekana kuwa na uhusiano na Afrika Kusini: Mnamo Agosti mwaka 2018, mamlaka ya Msumbiji ilimkamata raia mmoja wa Afrika Kusini André Mayer Hanekom, anayejulikana pia kama "Baba Mzungo", ambaye alihusika na kuwapelekea waasi silaha, dawa na pesa ambazo ziliwawezesha waasi hao kulipa mishahara ya wapiganaji wao. Mayer alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi mnamo Januari mwaka 2019 katika hali isiyoeleweka.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi
Rais wa Msumbiji Filipe NyusiPicha: picture-alliance/dpa/A. Silva

Kulingana na mwandishi wa habari wa mjini Valoi, kutekwa kwa bandari ya Mocímboa da Praia na waasi hao inamaanisha kwamba vikosi vya serikali kwa sasa vimeshindwa kuwadhibiti wanamgambo.

Mtaalamu wa masuala ya kisiasa nchini Msumbiji Dércio Alfazema amesema katika sehemu hii ya nchi, kwenye mkoa wa Cabo Delgado, kuna uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta ya malighafi barani Afrika kote. Mocímboa da Praia iko umbali wa kilomita 90 tu kutoka kwenye mradi wa mkubwa wa gesi asilia unaozihusisha kampuni za Ufaransa, Marekani, Italia na kampuni zingine za nishati.

Waziri wa ulinzi amesema serikali ya Msumbji haitawapa nafasi magaidi kudhibiti eneo lolote nchini humo na kuongeza kwamba haitakubalika kamwe eneo la Cabo Delgado litumbukie katika hali ya machafuko na ukiukaji wa haki za msingi za binadamu .

Vijiji vingi vimeteketezwa. Wale ambao hawawezi kukimbia wanakabiliwa na viitisho vya mara kwa mara au hata kuuliwa. Katika siku chache zilizopita, familia nyingi zimekimbia kutoka kwenye eno hilo kwa kuvuka bahari, au kwa kutumia mabasi, kupitia kwenye mpaka wa Pemba, katika mji wa Cabo Delgado. Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu elfu moja na mia tano wameuawa na wengine wapatao 250,000 wamekimbilia sehemu zingine za nchi. Mashambulio hayo yalianza mnamo 2017 huko Mocimboa da Praia na kuenea kwenye maeneo makubwa ya Cabo Delgado.

LINK: http://www.dw.com/a-54559570