1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump aanza ziara Afrika

Daniel Gakuba
3 Oktoba 2018

Melania Trump ameanza ziara ya siku tano barani Afrika, inayolenga kuhamasisha maisha bora kwa watoto.

https://p.dw.com/p/35ujB
Melania Trump Besuch in Ghana
Picha: picture-alliance/AP Photo/C. Kaster

Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump ameanza ziara ya siku tano barani Afrika, inayolenga kuhamasisha maisha bora kwa watoto.

Ziara yake ilianzia nchini Ghana alikowasili jana Jumanne na kutembelea hospitali ya mkoa. Katika Hospitali hiyo alishuhudia watoto wakipimwa uzito, na kupewa matone ya vitamini.

Bi Trump vile vile alikizuru kitengo cha hospitali hiyo cha watoto waliozaliwa kabla ya wakati. Akiwa mjini Accra, Melania Trump alipokelewa kwa mazungumzo na mke wa rais wa nchi hiyo  Rebecca Akufo-Ado na wakabadilishana zawadi.

Ziara hiyo ya Melania, ya kwanza barani Afrika kama mke wa rais wa Marekani, itamfikisha pia katika nchi za Malawi, Kenya na Misri.