1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yataka wanajeshi MONUSCO waondoke baada ya uchaguzi

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2023

Marekani imeonya kwamba ni mapema mno kuwaondoa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na badala yake imependekeza hatua hiyo ichukuliwe baada ya kumalizika uchaguzi wa Desemba 2023.

https://p.dw.com/p/4T6bW
DR Kongo | MONUSCO | Unrühen
Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Naibu Balozi wa Marekani nchini Kongo, Robert Wood, alisema kukiondoa haraka kikosi cha MONUSCO kunaweza kuacha pengo la usalama ambalo haliwezi kuzibwa na mamlaka za usalama za nchi hiyo.

Matamshi hayo ameyatoa wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Soma zaidi: MONUSCO walaani mashambulizi ya M23
Walinda amani wa UN watuhumiwa kutelekeza watoto Congo

Vikosi vingi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa barani Afrika vinakabiliwa na shinikizo la kuondoka kutoka kwa maafisa wa serikali na raia.

Baadaye wiki hii, Umoja wa Mataifa unakusudia kupiga kura ya kuamua hatima ya kikosi chake cha kulinda amani nchini Mali, MINUSMA.