1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani yasisitiza wito wa kusimamisha mapigano Gaza

4 Machi 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, amesisitiza umuhimu wa kusimamisha mapigano mara moja kwenye Ukanda wa Gaza na amesema sasa ni juu ya Hamas kukubali.

https://p.dw.com/p/4d8LC
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na mume wake Douglas Emhoff
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amesema ni juu ya Hamas kukubali kusitisha vita.Picha: Misper Apawu/AP/picture alliance

Harris amesema kutokana na hali mbaya iliyoko kwenye sehemu hiyo, ni lazima mapigano yasimamishwe. Wakati huo huo, makamu wa rais huyo wa Marekani atakutana na baraza la mawaziri wa Israel mjini Washington licha ya mawaziri hao kukemewa na Waziri Mkuu wao, Benjamin Netanyahu.

Benny Gantz, ambaye ni mpinzani mkuu wa kisiasa wa Netanyahu, anatarajiwa kufanya mazungumzo na maafisa kadhaa waandamizi wa utawala wa Biden, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na mshauri wa usalama wa taifa, Jake Sullivan.

Soma pia: UN yasema idadi kubwa walipigra risasi kituo cha msaada Gaza

Israel na Hamas wanajadiliana juu ya uwezekano wa kusimamisha mapigano na kuachiwa kwa mateka.