1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Marekani yashambulia maeneo ya Wahotuhi wa Yemen

Josephat Charo
12 Machi 2024

Vikosi vya Marekani vimesema vimeiharibu droni ya chini ya maji na karibu makombora 20 ya masafa marefu katika mfululizo wa mashambilizi dhidi ya waasi wa Houthi.

https://p.dw.com/p/4dQDJ
Marekani yajibu mashambulizi ya waasi wa kihouthi Yemen
Marekani yajibu mashambulizi ya waasi wa kihouthi Yemen Picha: Khaled Ziad/AFP/Getty Images

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM imesema katika taarifa jana usiku kuwa mashambulizi hayo yaliofanywa baada ya Wahouthi kufyetua makombora mawili kuilenga meli ya mizigo inayomilikiwa na Singapore kwa jina Pinocchio inayoendeshwa na Liberia.

CENTCOM imesema makombora hayo hayakuiharibu meli hiyo na hakukuwa na majeruhi wala uharibifu wowote ulioripotiwa. Waasi wa Houthi wamesema mapema leo katika taarifa yao kwamba waliishambulia meli hiyo, wakisisitiza kuwa shambulizi la kombora lililenga shabaha. Taarifa hiyo imeendelea kusema harakati za kijeshi zitaendelea kuongezeka wakati wa mwezi wa Ramadhani.