1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Milipuko yaripotiwa karibu na meli kwenye Ghuba ya Aden

Sylvia Mwehozi
9 Machi 2024

Shambulio linaloshukiwa kuwa la waasi wa Kihouthi nchini Yemen limesababisha milipuko karibu na meli kwenye Ghuba ya Aden.Milipuko hiyo inatokea baada ya kombora la Wahouthi kushambulia meli ya biashara Jumatano.

https://p.dw.com/p/4dKag
M/V Rubymar, ein unter Belize-Flagge fahrender britischer Massengutfrachter, der im Golf von Aden Öl ausläuft
Picha: US Central Command/AFP

Shambulio linaloshukiwa kuwa la waasi wa Kihouthi nchini Yemen limesababisha milipuko karibu na meli kwenye Ghuba ya Aden. Kituo cha operesheni za baharini cha jeshi la Uingereza, ambacho kinafuatilia njia za baharini za Mashariki ya Kati, kimesema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye meli hiyo, ambayo iliendelea na safari yake.Marekani yaharibu makombora 14 ya waasi wa Kihouthi

Milipuko hiyo ya jana Ijumaa inatokea baada ya kombora la Wahouthi kushambulia meli ya biashara katika Ghuba ya Aden siku ya Jumatano. Shambulio hilo liliwaua wafanyakazi watatu na wengine kulazimika kukimbia na kuitelekeza meli hiyo.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza vifo kuripotiwa katika kampeni ya mashambulizi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran kuhusu vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Wahouthi wanaelezea mashambulizihayo kama jaribio la kuishinikiza Israel kusimamisha vita.