Marekani yasema ndege zake tatu ziliangushwa kimakosa
2 Machi 2026
Jeshi la Marekani limesema ndege zake tatu za kivita ziliangushwa kimakosa kwa kushambuliwa na Kuwait hii leo, wakati wa shambulio la anga la Iran. Wafanyakazi wote sita waliondolewa salama kutoka ndege hizo aina ya F-15E Strike Eagles na wako katika hali nzuri.
Kulingana na taarifa ya jeshi la Marekani, ndege hizo ziliangushwawakati wa shambulizi la makombora na ndege za droni, lililokuwa likifanywa na Iran.
Lakini Televisheni ya taifa ya Iran, ilidai kwamba Tehran ililenga mojawapo ya ndege za Marekani ambayo ilianguka Kuwait bila kutoa maelezo ya kina. Taarifa ya Kamandi kuu ya Marekani ilisema Kuwait imekiri tukio hilo, kwamba mfumo wake wa ulinzi ulidungua ndege hizo kwa bahati mbaya kama sehemu ya usaidi wake katika operesheni ya Marekani nchini Iran.