1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Marekani: Yapo matumaini kuelekea amani nchini Ukraine

24 Novemba 2025

Ikulu ya White House imesema siku ya Jumapili kwamba mazungumzo kuhusu pendekezo la Marekani la kuvimaliza vita nchini Ukraine yalionyesha "matumaini makubwa."

https://p.dw.com/p/545WO
Marekani Washington D.C. 2025 | Ikulu ya White House mjini Washington, Marekani
Picha ya Ikulu ya White House mjini Washington, MarekaniPicha: Anna Rose Layden/UPI Photo/IMAGO

Ikulu ya White House aidha imethibitisha tena kwamba makubaliano yoyote ya baadaye "yatalenga kutetea kikamilifu" uhuru wa nchi hiyo.

Taarifa ya pamoja ya Marekani na Ukraine iliyotolewa na Washington baada ya mkutano mjini Geneva ilisema: kufuatia majadiliano hayo, pande hizo zimeandaa mfumo wa amani ulioboreshwa."

Mapema, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaamini watafikia malengo, ingawa hakutoa maelezo zaidi. 

Hata hivyo, washirika wa Ukraine barani Ulaya wamepinga namna mpango wa awali wenye vipengele 28 ulivyoandaliwa, ambao kwa kiasi kikubwa unaipendelea Urusi.

Kulingana na hati hiyo, Ukraine ingetakiwa kuikabidhi Urusi maeneo makubwa na kupunguza ukubwa wa jeshi lake, miongoni mwa hatua nyingine.