1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yamuondolea vikwazo kaimu Rais wa Venezuela

2 Aprili 2026

Marekani imeondoa vikwazo dhidi ya kaimu rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez, hatua inayotafsiriwa kama mabadiliko makubwa ya sera ya Washington kuelekea Caracas.

https://p.dw.com/p/5BY6r
Venezuela, Caracas 2026 | Rais wa mpito Delcy Rodríguez akutana na Waziri wa Nishati wa Marekani Chris Wright
Rais Delcy Rodriguez amesema hatua ya Marekani kuomdolea vikwazo ni muhimu kwa uhusiano.Picha: Juan Barreto/AFP

Hatua hiyo, iliyotangazwa na Wizara ya Fedha ya Marekani, inaashiria kutambuliwa rasmi kwa uongozi wa Rodríguez baada ya kuondolewa madarakani kwa kiomngozi wa nchi hiyo, Nicolás Maduro.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu uamuzi huo, lakini unaonekana kuwa sehemu ya juhudi za kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Rodríguez,ambaye aliwekewa vikwazo mwaka 2018, amepongeza hatua hiyo akisema ni mwanzo wa kuimarika kwa mahusiano na kufungua milango ya uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi nchini humo.

Marekani pia inatarajia kushirikiana na serikali mpya ya Venezuela kuongeza uzalishaji wa mafuta na rasilimali nyingine, huku nchi hiyo ikiwa na akiba kubwa zaidi ya mafuta duniani.