1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Marekani kuwahamisha raia wake kutoka Haiti kufuatia vurugu

17 Machi 2024

Marekani imetangaza kuwa imepanga kuwahamisha raia wake kutoka Haiti, kufuatia wiki kadhaa za ghasia za magenge ya uhalifu ambazo zimelikumba taifa hilo la Caribbean.

https://p.dw.com/p/4dpAP
Haiti | Uhalifu wa magenge ya uhalifu mjini Port-au-Prince
Machafuko kufuatia vurugu za magenge ya uhalifu nchini Haiti mjini Port-au-PrincePicha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Hakuna tarehe rasmi iliyotolewa na haijulikani ni Wamarekani wangapi watakaoweza kuhamishwa kutoka Haiti.

Ubalozi wa Marekani nchini Haiti umesema raia hao watahamishwa kutoka mji wa pili kwa ukubwa wa Cap-Haitien, wakati uwanja mkuu wa ndege katika mji mkuu wa Port-au-Prince ukiendelea kufungwa kutokana na machafuko hayo.

Serikali ya Guatemala imesema ofisi za ubalozi wake nchini Haiti zilivamiwa na  magenge hayo ya wahalifu ambayo yamekuwa yakishinikiza Waziri Mkuu Ariel Henry kuachia madaraka. Kiongozi huyo ametangaza siku ya Jumatatu kuwa atajiuzulu mara baada ya kuundwa kwa baraza la mpito.