1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo, Marekani zasaini makubaliano ya dola bilion 1.2.

27 Februari 2026

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Marekani zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya afya yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 1.2. ayo ni kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa Alhamisi.

https://p.dw.com/p/59VZb
Marekani na Kongo zimetiliana saini makubaliano ya afya ya dola za Kimarekani bilioni 1.2
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix TshisekediPicha: Fabrice Coffrini/AFP

Chini ya makubaliano hayo, Marekani itaipa Kongo dola milioni 900 katika kipindi cha miaka mitano. Fedha hizo zitatumika kuisaidia Kongo kupambana na UKIMWI, Kifua kikuu, malaria, vifo vya mama na mtoto na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Kongo yaahidi kuongeza bajeti yake ya Afya

Kongo kwa upande wake itaongeza bajeti yake ya afya kwa takriban dola milioni 300 ndani ya muda huo. Makubaliano hayo ni sehemu ya ushirika wa Marekani na nchi za Afrika katika sekta ya afya ambapo tayari mataifa 19 yameshasaini makubaliano ya aina hiyo. Mpango huo ni mbadala wa programu za afya zilizokuwa chini ya lililokuwa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID ambalo limefungwa.