1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Marekani: Wapiganaji wa Houthi wameishambulia meli ya Uswisi

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

Jeshi la Marekani limesema kwamba wapiganaji wa Kihouthi wa nchini Yemen, jana Jumatatu waliishambulia meli inayomilikiwa na Uswisi na iliyokuwa na bendera ya Liberia kwenye Ghuba ya Aden.

https://p.dw.com/p/4dApM
Meli ikiwaka moto baada ya waasi wa Houthi kushambulia kwa kombora katika Ghuba ya Aden
Meli Tanker Marlin Luanda ikiwaka moto baada ya waasi wa Houthi kushambulia kwa kombora katika Ghuba ya AdenPicha: Indian Navy /AP/picture alliance

Wanamgambo hao wa Kihouthi walifyatua makombora mawili na kuilenga meli inayomilikiwa na kampuni kubwa ya makontena ya MSC ya Uswisi. Ripoti za awali zinaonyesha kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya jana. Hata hivyo taarifa hiyo imeongeza kuwa kombora moja limesababisha uharibifu wa meli. Jeshi la Marekani pia limeripoti kwamba wanamgambo hao wa Kihouthi walifyatua kombora jingine tofauti katika Bahari ya Shamuna kuangukia majini. Wanamgambo hao wameapa kuzishambulia meli kwenye Bahari ya Shamu ambazo zinahusishwa na Israel, katika kampeni yake ya kushinikiza kukomeshwa kwa vita katika Ukanda wa Gaza.