1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Mamlaka ya kijeshi Myanmar yasisitiza kufanyika uchaguzi

9 Mei 2024

Mkuu wa jeshi la Myanmar amezungumzia mipango ya kufanya uchaguzi nchini humo na aliyekuwa kiongozi wa Cambodia Hun Sen katika mazungungumzo yao ya juma hili.

https://p.dw.com/p/4ffPf
Kiongozi wa kijeshi nchini Myanmar Min Aung Hlaing
Kiongozi wa kijeshi nchini Myanmar Min Aung HlaingPicha: Myawaddy/AP Photo/picture alliance

Hun Sen, ambaye alijiuzulu kama waziri mkuu wa Cambodia mwaka mmoja baada ya kuhudumu kwa takriban miongo minne, Jumanne alisema alimtaka kiongozi wa kijeshi Min Aung Hlaing kuzungumza na Mshindi wa Tuzo ya Nobel Aung San Suu Kyi, aliyegerezani na ambaye serikali yake iliondolewa katika mapinduzi ya 2021.

Soma pia:Mapigano yazuka kwenye mpaka wa Myanmar na Thailand

Lakini msemaji wa Kiongozi wa Kijeshi, Zaw Min Tun hakuzungumzia moja kwa moja pendekezo la kuzungumza na Suu Kyi ingawa mara kwa mara serikali ya kijeshi imeahidi kuirejesha Myanmar katika mkondo wa kidemokrasia pasipo kutoa muda wa kufanyika uchaguzi.