1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Mapigano yazuka kwenye mpaka wa Myanmar na Thailand

Tatu Karema
20 Aprili 2024

Mapigano yamezuka leo kwenye mpaka wa Myanmar na Thailand na kuwalizimisha takribani raia 200 kukimbia huku waasi wakipambana kuwafurusha wanajeshi wa nchi hiyo waliokuwa wamejificha katika kivuuko kimoja cha mpakani

https://p.dw.com/p/4f0Lf
Wanajeshi wa Thailand wakishika doria katika mpaka wa nchi hiyo na Myanmar mnamo Aprili 10 2024
Wanajeshi wa Thailand washika doria katika mpaka wa nchi hiyo na MyanmarPicha: AFP

Mashuhuda watatu kutoka pande zote za mpaka huo wa Myanmar na Thailand, wanasema walisikia mripuko mkubwa na milio ya risasi karibu na daraja hilo la kimkakati kutoka jana jioni na iliyoendelea hadi mapema leo.

Vyombo kadhaa vya habari vya Thailand vimeripoti kuwa takribani watu 200 kutoka Myanmar walivuuka mpaka kutafuta hifadhi ya muda nchini humo.

Soma pia:Wanajeshi wa Myanmar wajiondoa kwenye mji muhimu wa mpakani

Hata hivyo, ripoti hizo hazikuweza kuthibitishwa mara moja na msemaji wa jeshi hakupatikana kwa haraka kutoa tamko.

Waziri Mkuu wa Thailand, Srettha Thavisin, amesema anafuatilia kwa karibu hali hiyo na kwamba nchi yake iko tayari kutoa msaada wa kibinadamu, ikiwa itahitajika.