1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

ASEAN yatiwa wasiwasi na mapigano Myanmar

19 Aprili 2024

Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la mapigano nchini Myanmar.

https://p.dw.com/p/4exun
ASEAN Joko Widodo
Rais Joko Widodo akihudhuria mkutano wa ASEAN.Picha: Penny STEPHENS/ASEAN-Australia Special Summit 2024/AFPAFP

Kauli hiyo imetolewa baada ya kutokea hivi karibuni kwa mapigano ya kuwania kituo muhimu cha shughuli za biashara kilichoko katika eneo la mpaka wa Thailand. 

Mawaziri wa mambo wa ya nje wa Jumuiya hiyo wamezitolea mwito pande zote za mzozo huo kusitisha vurugu  nchini Myanmar ambako vita vimekuwa vikishuhudiwa  tangu jeshi lilipotwaa madaraka kwa nguvu mwezi Februari mwaka 2021. 

Soma zaidi: Thailand yaanza kupeleka misaada nchini Myanmar

Wiki iliyopita jeshi lililazimika kuondowa vikosi vyake katika kituo cha biashara cha Myawaddy baada ya siku kadhaa za mapambano na kundi la wanamgambo wa kabila la wachache linaloitwa Karen National Union (KNU) wanaoshirikiana na makundi mengine yanayolipinga jeshi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW