LRA kukutana na Museveni Alhamisi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

LRA kukutana na Museveni Alhamisi

Mkutano huo unatajwa kuwa ni wa aina yake kwa kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwa baadhi ya viongozi wa LRA kukanyaga Kampala katika kipindi cha miaka 21

Haya ndio baadhi ya matokeo ya mashambulizi ya LRA Kaskazini mwa Uganda,maelfu ya watu wameuwawa katika kipindi cha miaka 21 ya mapigano''

Haya ndio baadhi ya matokeo ya mashambulizi ya LRA Kaskazini mwa Uganda,maelfu ya watu wameuwawa katika kipindi cha miaka 21 ya mapigano''

Kundi la waasi wa kaskazini mwa Uganda la Lords Resistance Army LRA limesema litakuwa na mkutano huo wa aina yake pamoja na rais Yoweri Museveni mjini Kampala kesho alhamisi.

Mkutano huo utafanyika baada ya rais Museveni kurejea kutoka Marekani ambako alikutana na rais Gorge Bush na kuzungumzia kuhusu suala la amani kaskazini mwa Uganda.

Mkutano wa kesho utahudhuriwa na wajumbe wa ngazi ya juu ya kundi la LRA akiwemo mpatanishi mkuu wa kundi hilo Martin Ojul ambao watafika kwa mara ya kwanza mjini Kampala tangu kuanza kwa uasi kaskazini mwa nchi hiyo miaka 21 iliyopita ambapo maelfu ya watu waliuwawa na mamilioni ya wengine kuachwa bila makazi.Hata hivyo Joseph Kony kiongozi wa Kundi hilo hatahudhuria mkutano huo.

 • Tarehe 31.10.2007
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C77O
 • Tarehe 31.10.2007
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C77O
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com