LONDON:Watoto bado wanatembea na silaha nchini Jamhuri ya kidemkrasi ya Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 12.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Watoto bado wanatembea na silaha nchini Jamhuri ya kidemkrasi ya Kongo

Shirika linalotetea haki za binadamu duniani Amnesty International limesema kwamba maalfu ya watoto nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo bado wanadhibitiwa na makundi ya waasi wenye silaha.

Shirika hilo limeeleza kuwa hata baada ya miaka mitatu tokea kumalizika vita nchini humo watoto wapatao alfu 11 bado wana silaha mikononi.

Watu wapatao milioni nne waliuawa katika vita vya miaka mitano nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambapo watoto pia walitumika kama askari.

Watoto zaidi alfu 30 walihusishwa katika vita hiyvo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com