LONDON:Hatimaye Blair asema hadharani Saddam hakutendewa haki wakati aliponyongwa | Habari za Ulimwengu | DW | 10.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Hatimaye Blair asema hadharani Saddam hakutendewa haki wakati aliponyongwa

Waziri Mkuu wa Uingereza Tonny Blair amesema kuwa utaratibu uliyotumika kunyonga kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein haukuwa sahihi na haukubaliki.

Lakini hata hivyo Tonny Blair amesema kutokubalika kwa utaratibu huo, kusigubike uhalifu wa Saddam.

Hiyo ilikuwa ni mara kwa Waziri Mkuu huyo wa Uingereza kulaani hadharani utaratibu huo, ambapo walinzi walirekodi tukio hilo kupitia simu ya mkononi ikionesha Saddam akipewa maneno ya tashtiti kabla ya kunyongwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com