Loew kubakia kocha wa Ujerumani | Michezo | DW | 03.07.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Kombe la Dunia 2018

Loew kubakia kocha wa Ujerumani

Shirikisho la kandanda la Ujerumani (DFB) limethibitisha kuwa Joachim Loew atasalia kuwa kocha wa timu ya taifa na kuendelea kuisuka timu hiyo iliyoondolewa katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Kocha huyo ambaye ana mkataba wa hadi Kombe la Dunia la mwaka wa 2022, ameahidi kuifanyia mabadiliko makubwa timu ya taifa kwa kuwaondoa baadhi ya wachezaji wenye uzoefu ambao walionyesha mchezo mbaya sana katika michuano ya Urusi. Mkataba huo unarefusha uongozi wa Loew wa miaka 12 kama kocha wa Ujerumani. Katika kipindi hicho alipata mafanikio makubwa kama vile kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 na pia Kombe la Shirikisho mwaka 2017. Aidha, Ujerumani ilifika angalau nusu fainali ya mashindano mengine manne makuu.