1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kroos ashinda tuzo ya mchezaji bora

6 Agosti 2018

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza.

https://p.dw.com/p/32hfi
WM Russland 2018 I Deutschland vs Schweden - Toni Kroos
Picha: picture-alliance/AA/G. Balci

Haya ni kulingana na waandilizi wa tuzo hizo, jarida la kicker. Kroos ambaye alishinda kombe la champions league na Real Madrid mwezi Mei, alipata kura 185 kutoka kwa waandishi wa habari wa michezo na akamshinda mshambuliaji wa Freiburg Nils Petersen aliyepata kura 39 kisha beki wa Brazil anayeichezea Schalke, Naldo, akapata kura 38.

Mwaka jana Kroos alikuwa wa pili katika tuzo hizo zilizoshindwa na Philip Lahm ambaye walicheza pamoja katika klabu ya Bayern Munich na hata timu ya taifa ya Ujerumani. Jupp Heynckes amechukua tuzo ya kocha bora baada ya kuiongoza Bayern Munich kuishinda Bundesliga mwezi Mei kabla ya kustaafu.

Mwandishi: Jacob SafariReuters/AFP/DPA

Mhariri: Gakuba Daniel