1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Toni Kroos

Toni Kroos ni mchezaji soka wa kulipwa wa Ujerumani anaekipiga kama kiungo wa kati katika klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani.

Kroos alikuwa mchezaji wa timu za vijana za Ujerumani tangu akiwa na umri wa miaka 17 na alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya UEFA kwa umri wa chini ya miaka 17 mwaka 2006, na alishinda mpira wa dhahabu wa FIFA katika kombe la dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 17. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichofika nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2010 na UEFA Euro 2012. Pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.