1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Toni Kroos kutundika daluga baada ya EURO 2024

21 Mei 2024

Mchezaji kiungo wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani Toni Kroos amesema atastaafu kucheza soka baada ya mashindano ya kombe la EURO 2024 yatakayoanza Juni 14 hadi Julai 14 hapa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4g6Gf
Kiungo wa Ujerumani, Toni Kroos
Kiungo wa Ujerumani, Toni KroosPicha: eu-images/IMAGO

Toni Kroos atatundika njumu zake na kufikisha mwisho taaluma yake ya kucheza soka baada ya michuano ya kombe la EURO 2024. Mchezaji huyo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani amesema katika ujumbe wake.

Kiungo Kroos, mwenye umri wa miaka 34, alishinda kombe la dunia la kandanda mnamo 2014 na Ujerumani na alirejea katika kikosi cha timu ya taifa baada ya kukaa nje kwa miaka mitatu ya kustaafu mwezi Machi kuisaidia timu ya taifa katika michuano ya kombe la EURO 2024 kuanzia Juni 14 hadi Julai 14.

Kroos alishinda mataji matatu ya Bundesliga na makombe matatu ya shirikisho la Ujerumani DFB Pokal, yakiwemo mataji matatu mwaka 2013, na Bayern Munich na mataji mengine mengi tangu alipohamia Real Madrid 2014, yakiwemo mataji manne ya ligi ya mabingwa Ulaya, Champions, makombe matano ya kombe la dunia la vilabu pamoja na mataji manne ya La Liga na taji moja la Coppa del Rey.

Kroos atacheza mechi mbili nyingine na Real Madrid, mechi ya fainali ya La Liga dhidi ya Real Betis na mechi ya fainali ya kombe la mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund. Kwa Ujerumani, atakuwa na mechi tatu za makundi za kombe la EURO 2024 dhidi ya Scotland, Hungary na Uswisi na pengine mechi zaidi.

(dpae)