1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kosa ni kosa

13 Septemba 2018

Sakata la mapadiri kuwadhalilisha watoto wengi kingono nchini Ujerumani limezua mashaka na kulichafua kanisa katoliki katika taifa hilo la Ulaya.Kiasi watoto 3677 inasemekana wametendewa ukatili huo na mapadiri

https://p.dw.com/p/34p5b
USA Seattle Betende Menschen
Picha: picture-alliance/ZUMA Wire/P. C. Gordon

Utafiti uliofanywa na Baraza la Maaskofu wa Ujerumani juu ya udhalilishaji wa kingono kwenye Kanisa Katoliki ni jambo zuri, lakini halitoshi, anasema Christoph Strack wa DW anayehoji kwamba lazima waliotenda wakabiliwe na matokeo ya uovu wao na taasisi ya ukasisi lazima iwe na uadilifu.

Si takwimu zote katika utafiti huu ni mpya lakini ukubwa wa idadi iliyotolewa umepindukia kiwango cha kuogofya.

Kadinali Marx ndiye mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Ujerumani na kimya chake juu ya kusambaa kwa kadhia hizi ndani ya kanisa hilo nchini Marekani juu ya suala hili hili kilitowa ishara ya wazi kwamba kuna takwimu mpya ya idadi ya wahanga katika utafiti ulioitishwa na makasisi wa Kijerumani.

Kwa bahati mbaya sana kwamba idadi hiyo haitokuwa ya mwisho kwa sababu sio majalada yote yaliyowasilishwa mezani.

Uchunguzi uliofanyika ulilenga tu makbrasha ya kumbukumbu za dayosisi na kwa maana hiyo waliolengwa kwenye uchunguzi huu ni mapidiri wa dayosisi tu. Lakini mapadiri wanaohusika kwenye shule, masuala ya watoto na makundi ya vijana bado hawajamulikwa.

Kingine kinachopaswa kufahamika ni kwamba hakuna wachunguzi wa kiserikali wanaoruhusiwa kuchunguza masuala ya kikanisa. Wajerumani wanafahamika sana kwa kuwa waadilifu.

DW Intranet Christoph Strack
Christoph Strack-Mwandishi wa DWPicha: DW

Mwaka 2014, makasisi wa Kikatoliki nchini Ujerumani walipanga kufanya uchunguzi kamili wa kisayansi. Ni kanisa tu ndilo lililohusika kutoa jukumu la kufanyika uchunguzi huo, serikali haikuhusishwa.

Wakati huo viongozi wa Kanisa Katoliki, ambao bado wakimulikwa na kadhia za ubakaji watoto wadogo zilizoibuka nchini Ujerumani mwanzoni mwa mwaka 2010, walizuia hatua ya serikali kuhusishwa kwa kiasi kikubwa katika uchunguzi.

Nchini Marekani waendesha mashtaka kwa idadi kubwa kabisa katika majimbo ya nchi hiyo   wanachunguza kwa hivi sasa visa vya unyanyasaji kingono katika Kanisa Katoliki.

Kwa hivyo, Kanisa hilo huenda likapata mshangao mkubwa zaidi na, hapana shaka, suala hili litawagusa watu wengi katika uongozi wa juu kabisa wa taasisi hiyo ya kidini.

Mjadala kuhusu kadhia za ngono pamoja na wafanyakazi wa kanisa na mfumo wa kimadaraka katika kanisa hilo ni lazima uendelee.

Ripoti ya uchunguzi iliyotolewa ni hatua moja ya kusogea mbele lakini pia Kanisa Katoliki linapaswa kuwa wazi katika masuala ambayo ni pamoja na utekelezwaji wa sera ya kutoruhusu kabisa vitendo hivyo.

Makao makuu ya kanisa hilo, Vatikan, yameshatangaza kwamba Papa Francis amewaalika viongozi wa mabaraza 80 ya makasisi duniani kushiriki kwenye mkutano utakaofanyika mwezi Februari 2019.

Lakini kikubwa watu wanachobidi kukifahamu ni kwamba visa vya unyanyasaji kingono unaofanywa na mapadiri havikutokea Ujerumani na Marekani tu, bali pia nchini Poland na Italia, Afrika, Asia na Australia.

Mwandishi: Saumu Mwasimba/Christoph Strack

Mhariri: Mohammed Khelef

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW