1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yamtaja Mmarekani wa 3 aliyehusika jaribio la mapinduzi

Sylvia Mwehozi
22 Mei 2024

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Brigedia Jenerali Sylvain Ekenge, ametaja jina la Mmarekani wa tatu aliyehusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa mjini Kinshasa.

https://p.dw.com/p/4g7rh
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |  Kinshasa
Mmoja wa washambuliaji waliovamia ikulu ya rais mjini KinshasaPicha: Christian Malanga/Handout/REUTERS

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Brigedia Jenerali Sylvain Ekenge, ametaja jina la Mmarekani wa tatu aliyehusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa mjini Kinshasa.

Jenerali Ekenge amelieleza shirika la habari la The Associated Press kuwa mshambuliaji huyo wa tatu ametambulika kwa majina ya Taylor Thomson.

Haikuweza kufahamika mara moja ikiwa Thomson ni miongoni mwa watu waliokamatwa au kuuawa siku ya Jumapili kufuatia shambulio la kwenye Ikulu ya rais na jingine kwenye makazi ya mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi.Risasi zarindima nyumbani kwa mwanasiasa wa Kongo Vital Kamerhe

Wakati huo huo familia ya kiongozi wa shambulio hilo Christian Malanga imekusanyika mjini Utah Marekani, kuomboleza kifo chake baada ya kuuawa katika majibizano ya risasi. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema haiwezi kuthibitisha ikiwa Malanga ni raia wa nchi hiyo.