1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Kongo lasema limezima ´jaribio la mapinduzi´

19 Mei 2024

Jeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limesema hii leo kwamba limezima jaribio la mapinduzi karibu na ikulu ya nchi hiyo mjini Kinshasa yaliyopangwa na "Wakongamani na raia wengine wa kigeni".

https://p.dw.com/p/4g3KV
Maafisa usalama wa Kongo
Maafisa wa usalama wa Kongo wakishika doria kwenye eneo inakoarifiwa jaribio la mapinduzi limesambaratishwa. Picha: Arsene Mpiana/AFP

Katika ujumbe kupitia televisheni msemaji wa jeshi Jenerali Sylvain Ekenge amesema jaribio hilo limezuiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.

Ameuhakikishia umma wa Kongo kwamba wale waliopanga njama hiyo wamedhibitiwa bila hata hivyo kufafanua iwapo wamekamatwa au wameuawa.

Jaribio hilo la mapinduzi lilianza mnamo majira ya asubuhi nje ya maakazi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi Vital Kamerhe yaliyopo karibu na ofisi za rais Felix Tshisekedi.

Milio la risasi ilisikika na duru zikaarifu kuwa watu wenye silaha walipambana kwa bunduki na walinzi wa Kamerhe. Hivi sasa hali ya utulivu imerejea lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu mkasa huo.