Kinshasa:Makaburi ya Halaiki yagundulikana huko Kongo. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinshasa:Makaburi ya Halaiki yagundulikana huko Kongo.

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamegundua makaburi walimozikwa halaiki ya watu katika mkoa wa mashariki wa Ituri, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Taarifa zilisema makaburi hayo yalikua na jumla ya maiti 30.

Wengi ni wanawake na watoto ambao walipotea mapema mwaka huu na sasa inafikiriwa huenda waliuwawa kati ya Agosti na Oktoba.

Maafisa wawili wa polisi wamekamatwa kuhusiana na kutoweka kwa watu hao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com