1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Kagame ahofia utata wa Marekani kwa wahanga wa mauaji

Lilian Mtono
8 Aprili 2024

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba alikuwa na wasiwasi wa kile anachokiona kama kushindwa kwa Marekani kuyatambua mauaji ya Mauaji ya 1994 kama mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi walio wachache nchini humo.

https://p.dw.com/p/4eYP4
Ruanda Kigali | Gedenkfeier 30 Jahre nach Völkermord
Picha: LUIS TATO/AFP

Kagame amewaambia waandishi wa habari kwamba suala hilo lilikuwa ni "mada ya mazungumzo" walipokutana na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton aliyeongoza ujumbe wa Marekani nchini Rwanda kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji hayo.

Raia wengi wa Rwanda walimkosoa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwa kushindwa kuweka wazi kwamba mauaji hayo ya kimbari yaliwalenga Watutsi, alipoandika kwenye ukurasa wa X kuhusiana na maadhimisho hayo.

Kagame amesema anaamini alifikia makubaliano na maafisa wa Marekani muongo mmoja uliopita wa kutoyakosoa mauaji hayo wanapofanya kumbukumbu hiyo.  

Wahutu wenye misimamo mikali waliwaua karibu Watutsi 800,000, wengi wao wakiwa ni Watutsi, katika kampeni iliyochochewa na serikali.