Migogoro
Iran yazikamata meli mbili kwenye Mlango Bahari wa Hormuz
22 Aprili 2026
Matangazo
Kulingana na shirika la habari la Tasnim, jeshi la Walinzi wa Mapinduzi limezikamata meli hizo kutokana na kukiuka sheria za baharini na lilizisindikiza hadi kwenye fukwe za Iran.
Ni meli za kwanza kukamatwa tangu kuanza kwa vita
Hii ni mara ya kwanza Iran kukamata meli katika eneo hilo tangu vita vilipoanza mwishoni mwa mwezi Februari. Awali, jeshi la Iran liliripoti kuzishambulia meli tatu za makontena kwenye Mlango Bahari wa Hormuz ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Haya yanajiri wakati ambapo Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kusitisha mashambulizi dhidi ya Tehran kwa muda usiojulikana, kufuatia ombi kutoka kwa wapatanishi wa Pakistan ili kupisha mazungumzo ya usuluhishi.