1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Tunarejea kwenye usitishaji mapigano Ukanda wa Gaza

30 Oktoba 2025

Jeshi la Israel limetangaza kuendelea na usitishaji wa mapigano kwenye Ukanda wa Gaza muda mfupi baada ya kufanya mashambulizi makali yaliyowaua zaidi ya Wapalestina 100.

https://p.dw.com/p/52otB
Baadhi ya Wapalestina wakikagua jengo lililoshambuliwa na Israel katika jiji la Gaza
Ukanda wa Gaza Oktoba 29.10.2025Picha: Ebrahim Hajjaj/REUTERS

Miongoni mwa waliouwawa ni wanawake na watoto 66 kulingana na mamlaka za ukanda huo. Mashambulizi hayo ndiyo makubwa zaidi tangu yalipoanza kutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita Oktoba 10.

Israel, Hamas zashutumiana kukiuka makubaliano ya kusitisha vita

Israel ilianza kufanya mashambulizi kwa madai kuwa kundi la Hamas lilikiuka makubaliano hayo. Hata hivyo kundi hilo limekanusha na kusema Israel ndiyo iliyokiuka makubaliano.