1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je Ulaya yahitaji kutangaza "uchumi wa wakati wa vita"?

31 Mei 2023

Udhibiti wa viwanda? Kudhibiti bei? Mgao wa chakula? Je kamishna wa Umoja wa Ulaya Thiery Breton alimaanisha nini aliposema “uchumi wa vita“?

https://p.dw.com/p/4S1eJ
Bundeswehr Patronen
Picha: Björn Trotzki/IMAGO

Maneno yanayotumika kwa kubadilishana kama "uchumi wa vita” au "uchumi wa wakati wa vita” hurejesha kumbukumbu za enzi mbaya zilizopita ambapo serikali zilipanga upya mifumo yao ya kiuchumi na matokeo ya kiviwanda huku zikitanguliza uzalishaji kwa juhudi za kivita. Swali linaloibuka kwa sasa ni je ipo haja kwa Ulaya kutangaza ‘uchumi wa wakati wa vita'? 

Kamishna wa Umoja wa Ulaya Thierry Breton alianza kutafakari kuhusu dhana hiyo mwanzoni mwa Machi, alipokuwa akitafuta hatua za kuboresha kwa haraka maagizo ya serikali za Umoja wa Ulaya za kutengenezwa kwa silaha za kuipa Ukraine na pia kuongeza akiba zao.

Scholz: Silaha zinazotolewa na Ujerumani kwa Ukraine hazitakiwi kushambulia ardhi ya Urusi

Kamishna huyo amezuru zaidi ya vituo kumi vinavyotengeneza silaha katika Umoja wa Ulaya, ambapo alipata malalamiko ya ukosefu wa kusainiwa kwa kandarasi au mikataba ya muda mrefu. Licha ya maamuzi ya Umoja wa Ulaya kuongeza ufadhili na kupunguza vizuizi vya ununuzi wa pamoja, juhudi zinaendelea polepole sana.

Thierry Breton, kamishna wa Umoja wa Ulaya
Thierry Breton, kamishna wa Umoja wa UlayaPicha: John Thys/AFP/Getty Images

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari mnamo Mei 3, Breton alisema ucheleweshaji huo hauendani na mahitaji yao ya haraka. Alisema kuna haja ya kuongeza matengenezo ya silaha viwandani kuelekea kile kinachoitwa uchumi wa "wakati wa vita”.

Je maneno yake hayakuruhusiwa?

Lakini yaonekana Breton hakushauriana na nchi zote wanachama wa umoja huo ikiwa angeruhusiwa kuyatumia maneno hayo katika ufafanuzi wake wa hali ilivyo.

Ujerumani kuipatia Ukraine msaada wa kijeshi wa euro bilioni 2.7

Huenda Ujerumani ndiyo inauona mtizamo huo kuwa tete zaidi. Balozi wake nchini Poland Thomas Bagger anafahamu mawili matatu kuhusu shinikizo la kupeana silaha. Anaitizama mbinu ya Breton kukosa tija. "Hutakuwa na jibu chanya kwa maneno 'uchumi wa vita' nchini Ujerumani, sio njia sahihi ya kuhamasisha juhudi." Bagger alisema kwa ufupi katika Mkutano huko Tallinn, Estonia mapema mwezi Mei.

NATO yajadili jinsi ya kuipatia Ukraine silaha zaidi

Edward Lucas, mchambuzi katika kituo cha Sera za Ulaya (CEPA) amesema mwenyewe angepiga marufuku kauli hiyo kwa kuwa ina maana tofauti katika nchi mbalimbali. Ameliambia shirika hili la habari DW kwamba uchumi kamili wa vita ni pale watu wenye bunduki huingia viwandani na kuvilazimisha kutengeneza silaha zaidi.

Nchini Ujerumani, Lucas ameliambia DW kwamba maneno hayo hukumbusha jinsi utawala wa Manazi ulivyodhibiti uchumi pamoja na mateso ya wengi na dhuluma dhidi ya watumwa.

Mchambuzi mwengine Ben Tallis kutoka Baraza la Ujerumani la Mahusiano ya Nje (DGAP) amesema rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia amewahi kuzungumzia uchumi wa vita lakini bila ya kuhusisha vipengele vyake tete.

Ukraine yahitaji silaha zaidi kuliko idadi ambazo Marekani na Umoja wa Ulaya zinaweza kuwapa kwa sasa.
Ukraine yahitaji silaha zaidi kuliko idadi ambazo Marekani na Umoja wa Ulaya zinaweza kuwapa kwa sasa.Picha: Diego Herrera Carcedo/AA/picture alliance

Maneno "Uchumi wa wakati wa vita" waweza kufasiriwa visivyo

Nathanie Tocci anayesimamia taasisi ya Italia kuhusu masuala ya kimataifa amesema ni muhimu kutoa ishara ya haja hiyo kwa Umoja wa Ulaya na kwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Amesema inaeleweka ni kwa nini maafisa wa Umoja wa Ulaya wanajaribu kutumia dondoo hiyo kwa kuwa wanahitaji kuziba pengo kubwa katika mtizamo wa vitisho kote Ulaya, kushawishi nchi wanachama ambazo ziko mbali sana na mstari wa mapambano, kwamba badala ya kutumia fedha kwenye masuala ya ndani, wanapaswa kuzitumia kwenye sekta ya ulinzi kutuma silaha Ukraine. Tocci ameeleza kuwa baadhi tayari wanaunga mkono wazo hilo lakini muda zaidi huhitajika kufanya wengine kuikumbatia hoja hiyo.

Kwa upande mwingine waziri wa Ulinzi wa Estonia Hanno Pavkur, amesema hakuna mtu anayepaswa kutaka matumizi ya msemo ‘uchumi wa vita' nchini mwake, taifa ambalo tayari limetoa zaidi ya asilimia moja ya Pato lake la Taifa kama msaada kwa Ukraine.

Mwandishi: