1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Kiarabu yakabiliana na itikadi kali mtandaoni

Saleh Mwanamilongo
15 Julai 2020

Baada ya kuibuka kwa kundi la "Dola la Kiislamu", mataifa kadhaa ya Kiarabu yalibuni hatua za kuvuruga maudhui za itikadi kali mtandaoni. Lakini shughuli zao zimezusha wasiwasi kuhusu jukumu lao la kupambana na ugaidi.

https://p.dw.com/p/3fMqp
Vereinigte Arabische Emirate | Skyline im Fenster
Picha: picture-alliance/AFP Creative/M. Naamani

Chini ya miaka mitano iliyopita, ujumbe wa IS kwenye mitandao ulizilazimisha serikali za Marekani na nchi za Kiarabu kufikiria kuhusu mtizamo wao kutokana na ujumbe wa itikadi kali mitandaoni. Hali hiyo ilisababisha kuwepo mipango kadhaa, ikiwemo iliyofanywa kwa ushirikiano na Marekani.

Moja wapo ni kituo cha Sawab kinachohusika na juhudi za ujumbe wa mtandaoni, kilichozinduliwa mwaka 2015 na kimeongozwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, katika kuunga mkono juhudi za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kupambana na IS.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya utafiti ya bunge la Marekani, kikiwa na bajeti ya dola milioni sita ambazo ni sawa na Euro milioni 5, pamoja na wafanyakazi kadhaa, kituo hicho kimekuwa kikitoa taarifa zake na idara za kiusalama za kimataifa, mara familia zinaporipoti kuhusu visa vya itikadi kali.

Mwaka 2017, Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Mfalme Salman wa Saudi Arabia, aliongoza mpango mpya wa kuanzisha kituo cha ulimwengu kupambana na itikadi kali kinachoitwa Etidal.

Changamoto za kukabiliana na ujumbe wa itikadi kali

Wakati huo Trump alikipa kituo hicho jukumu la kupambana na itikadi kali kwa ajili ya kuimarisha Uislamu wenye msimamo wa wastani kwenye nchi washirika za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, na hata Qatar. Lakini mradi huo umeonekana kuwa haufai.

USA Washington | Barack Obama und Scheich Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan
Kituo cha Sawab kilizinduliwa kwa msaada wa Marekani kama "operesheni ya ushiriki na ujumbe wa mtandaoni" yenye lengo la kupambana na IS.Picha: picture-alliance/AP Photo/C. Kaster

Ukurasa wa Sawab katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa lugha za Kiingereza na Kiarabu, una wafuasi milioni 1.6, lakini kanda zake za video kwenye mtandao wa YouTube zinatizamwa miezi ya hivi karibuni na watu wasiozidi kumi.

Juhudi za hivi karibuni za kituo cha Etidal ni pamoja na jukwaa la ''msimamo wa wastani'' linalolenga kuzisaidia familia kuchangia katika kupambana na ujumbe wa itikadi kali kwenye mitandao ya kijamii, lakini jukwaa hilo ni aina ya mawasiliano ya mtandaoni, ambayo haijulikani wapi taarifa hizo zinakwenda na nani anazishughulikia.

Kituo cha Sawab kilisherehekea kufikia wafuasi milioni 8 kwenye mitandao ya kijamii, huku Etidal ikielezea kwamba mitambo yake inachukuwa tu sekunde 6 kwa kufahamu ujumbe wenye itikadi kali. Lakini vituo vyote viwili vilishindwa kutoa ushahidi wa utendaji kazi wao bora. Juhudi za DW kupata maelezo kutoka vituo hivyo viwili hazikufua dafu.

Ni wazi kwamba ni vigumu kutathmini miradi ya aina hiyo. Kwenye ripoti yake mwaka 2016, wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ilielezea tatizo la kujaribu kufahamu ikiwa kuna mabadiliko ya tabia au vitendo.

Eric Rosand wa shirika la utafiti la Taasisi ya Brookings mjini Washington, anasema kwamba jamii ya wataalamu imebaini kwamba ajenda ya nchi za Kiarabu imekwenda mbali zaidi kuliko kazi inayofanywa na Etidal na Sawab.

Lakini kuna baadhi ya serikali ambazo hazikufanya chochote katika juhudi za kujipatia sifa nzuri kwenye nchi za Magharibi.

Ripoti ya mwaka 2018 ya Kituo cha Marekani cha American Progress, ilisema kwamba Etidal na Sawab zilifanya kazi ili kuzipa nafasi nzuri nchi hizo kama viongozi bora wanaokuza Uislamu wa wastani na wanaopambana na itikadi kali, hali ambayo inakadiriwa ulimwenguni kote, lakini imeundwa mahsusi kwa mataifa ya Magharibi.

Chanzo: DW