ISTANBUL:Mgombea binafsi apigwa risasi na kufa Uturuki. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISTANBUL:Mgombea binafsi apigwa risasi na kufa Uturuki.

Mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu wa tarehe 22 mwezi huu nchini Uturuki Tuncay Seyranlioglu ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Istanbul.

Tuncay mwenye umri wa miaka 41 alipigwa risasi wakati akiwa ndani ya gari lake baada ya kutoka kwenye kipindi cha mahojiano cha televisheni, ambapo alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

Polisi wa Uturuki inawashikilia watu watatu kuhusiana na tukio hilo.Uchaguzi wa bunge nchini Uturuki unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ambapo chama cha Waziri Mkuu Erdogan cha AKP kinatarajiwa kupata ushindi.

Wakati huo huo Waziri Mkuu huyo recep Tayyip Erdogan amesema kuwa atang´atuka katika ulingo wa siasa iwapo chama chake kitashindwa katika uchaguzi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com