1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ kutolea uamuzi kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel

24 Mei 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ilitarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini kutaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya Israel ili kuzuia mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

https://p.dw.com/p/4gEi6
Majaji wa Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ).
Majaji wa Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ).Picha: Nick Gammon/AFP/Getty Images

Uamuzi huo uliotarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa (24 Mei) mjini The Hague unahusu uwezekano wa kuagiza kuondolewa mara moja kwa jeshi la Israel kutoka mji wa wa Rafah ulio kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Soma zaidi: Mahakama ya ICJ yatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu vita vya Gaza

Rais wa mahakama hiyo, Nawaf Salam, ambaye ni mwanasheria kutoka Lebanon, ndiye aliyetarajiwa kuusoma uamuzi huo.

Afrika Kusini ililitetea shauri lake mbele ya ICJ kwa hoja kwamba hatua za awali za mahakama hiyo kuhusiana na vita vya Gaza hazikuwa zikitosha.

Soma zaidi: ICJ kuamua juu ya kuondoka kwa vikosi vya Israel mjini Rafah

Israel imekanusha madai yote dhidi yake, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akitumia suala la haki ya nchi yake kujilinda katika kujibu mashambulizi ya wanamgambo wa Kipalestina dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7.