1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hungary yafungia tovuti 12 za habari za Ukraine

29 Septemba 2025

Hungary imetangaza leo kufungia ufikiaji wa tovuti 12 za habari za Ukraine baada ya hatua kama hiyo kuchukuliwa na Ukraine na kuzidisha mvutano kati ya mataifa hayo mawili jirani.

https://p.dw.com/p/51FGN
CPAC Hungary 2024 |  Viktor Orban
Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor OrbanPicha: Szilard Koszticsak/MTI/AP/Picture Alliance

Katika chapisho kwenye mtandao wa facebook hii leo, mkuu wa wafanyakazi wa serikali ya waziri mkuu wa Hungary, Gergely Gulyas, amesema nchi huru lazima itoe jibu sawa kwa shambulio lisilokuwa na msingi.

Hungary yatoa sababu za kufungiwa kwa tovuti zake na Ukraine

Gulyas amesema Ukraine ilipiga marufuku tovuti za Hungary kwa sababu zilikosoa vikwazo dhidi ya Urusi na msaada wa kijeshi kwa Ukraine, pamoja na kuukosoa Umoja wa Ulaya na muungano wa kujihami wa NATO kwa kuwa na mgawanyiko na kutofanya kazi.

Pia amesema ikiwa mgawanyiko wa Umoja wa Ulaya unatoa sababu ya udhibiti wa serikali nchini Ukraine, basi ni wakati kwa Ukraine kufutilia mbali azma yake ya kujiunga nao.

Ukraine haikutoa jibu la haraka la hatua hiyo ya Hungary.