Hali ya uchumi nchini Kenya | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hali ya uchumi nchini Kenya

Homa ya uchaguzi imeshaanza kupanda nchini Kenya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ujao wa rais.

Markiti mjini Nairobi

Markiti mjini Nairobi

Nchini kenya joto la uchaguzi mkuu hapo mwakani limeanza tena,serekali ilioko madarakani ya Rais Kibaki ikitarajia kuchaguliwa tena na wananchi; kwa kua uchumi wa Kenya umekuwa katika kipindi

Hichi cha Awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Mwai Kibaki.

Lakini baadhi ya wakenya wanasema hapana lilobadilika ispokua watu kuzidi kununua Airtime (kadi za kuongeza muda wamazungumzo katika simu zao za mkononi)

Takwiimu zinaonyesha Rais Mwai Kibaki alipochaguliwa Rais wa kenya mwaka 2002 uchumi wa nchi hio ulikua 0.3% lakini kufikia mwaka 2005 ukuwaji wa uchumi uliongezeka kwa 5.8% hadi 6% mwaka jana.

Mfanyabiashara Manu Chandaria wa kiwanda cha kutengeneza Mabati anasema ongezeko hilo la ukuwaji wa kiuchumi umemuwezesha kutengeneza Mabati zaidi kwa soko la mataifa ya njee na sasa wako katika majadiliano ya kuuza mabati yatakayofikia dollar million 30.

Bw Samuel Ochieng Mkurugenzi mkuu wa shirika la kibinafsi lenye mtandao wa kutoa

bure maelezo ya kiuchumi anasema , watu wenye tabaka la juu ambao ndio wachache wanafurahikia ukuwaji huo, kwa sababu ndio hao hao wanaomiliki uchumi huo, na hali walala hao ambao ndio wengi hawafaidiki chochote .

Nae Havi Murungi mkurugenzi anaefanya utafiti wa kiuchumi anakubaliana na maoni ya Bw Ochieng na kusema kua bidhaa nyingi zinazo uuzwa na huduma inayotolewa vyote vinalingana na idadi ya hao wachache wenye uwezo .

Katika utafiti wake Murungi anasema Suala la simu za mkononi (mobile phones) watu kununua Air time (kadi za kuongeza muda wa mazungumzo) gharama yake imekua ikipanda

Sasa itakuaje bidhaa nyengine zishuke bei?

lakini serekali inasisitiza mambo ni poa kabisa ,idara ya takwimu ya taifa in kenya inasema, 46% ya watu sasa wanaishi katika hali ya umaskini ukilinganisha na 52.3% miaka 10 iliopita .

Kwa mujibu wa repoti ya shirika la umoja wa mataifa 2006 kuhusu maendeleo ya binaadamu United nation Human Development , 23% raia wa kenya

Huishi kwa chini ya dollar moja kwa siku na 58% huishi kwa chini ya dollar mbili kwa siku.

Taasisi ya kibinafsi inayohusika na masuala ya kiuchumi Inst of Economic Affairs inasema tatizo linaloikabili serekali ya Rais Mwai Kibaki kwa sasa, ni kuboresha miundo mbinu ,na hali ya usalama kutokana na wizi wa kutumia silaha ,uporaji wa magari na pia kuweko wahuni wengi, yote hayo huleta khofu kwenye jumuia ya wafanya biashara.

Pia rushwa imekithiri nchini humo kiasi kwamba linawavunja moyo wanaotaka kuanzisha vitega uchumi wandani na walioko njee ya kenya amesema Micheal Renneberger balozi wa US nchini kenya.

Wakati Rais Kibaki alipoingia madarakani aliahidi kupiga vita ulaaji rushwa nchini kenya na hasa suala la Kampuni bandia ya Anglo leasing iliopewa kandarasi ya Mamillioni ya Dollar, kutengeneza Passpoti zisizoweza kughushiwa na pia kujenga Maabara ya idara ya polisi, yote hayo yanaisubiri serekali ya Rais kibaki kabla ya uchaguzi mkuu wa urais

hapo mwakani.

 • Tarehe 09.05.2007
 • Mwandishi Omar Mutasa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHEa
 • Tarehe 09.05.2007
 • Mwandishi Omar Mutasa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHEa
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com