1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Friedrich Merz wa CDU afuta kauli ya kushirikiana na AfD

Bruce Amani
24 Julai 2023

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Ujerumani cha CDU Friedrich Merz amefuta kauli zake za awali kuwa yuko tayari kufanya kazi na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD katika ngazi ya mtaa.

https://p.dw.com/p/4UJ7C
Friedrich Merz entlässt Generalsekretär Mario Czaja
Picha: Frederic Kern/Geisler-Fotopress/picture alliance

Kati mahojiano ya mwishoni mwa wiki na chombo kimoja cha habari cha Ujerumani, Merz alisema kama mgombea kutoka chama cha AfD angeshinda wadhifa wa mkuu wa ulaya au meya, ni kawaida kutafuta mbinu za kuendelea kufanya kazi katika mji huo.

Ijapokuwa Merz alifuta uwezekano wa kufanya kazi na AfD katika ngazi ya majimbo ya shirikisho au katika Bunge la Ulaya, kauli zake zilichochea ukosoajikutoka chama cha CDU na mshirika wake Christian Social Union - CSU.

Soma pia:Chama cha siasa kali cha AfD chashika nafasi ya pili Ujerumani

Ameandika kwenye Twitter kuwa msimamo wa CDU bado ni ule ule. Hakuna ushirikiano wowote kati ya CDU na AfD katika ngazi ya mabaraza ya miji.

AfD ni chama cha siasa kali za kizalendo kinachopinga sera za uhamiaji.