1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA kujadili ombi la kuisimamisha Israel soka la kimataifa

17 Mei 2024

Shirikisho la soka duniani FIFA litatafuta ushauri wa kisheria kabla ya kuandaa kikao maalumu kufikia tarehe 20 mwezi Julai, kufanya maamuzi juu ya pendekezo la Palestina la kuisimamisha Israel kwenye soka la kimataifa.

https://p.dw.com/p/4fyeb
Rais wa FIFA Gianni Infantino,
Rais wa FIFA Gianni InfantinoPicha: William West/AFP

Shirikisho la soka duniani FIFA litatafuta ushauri huru wa kisheria kabla ya kuandaa kikao maalumu kufikia tarehe 20 mwezi Julai, kufanya maamuzi juu ya pendekezo la Palestina la kuisimamisha Israel kwenye soka la kimataifa kwa sababu ya mzozo wake na kundi la wanamgambo la Hamas.

Soma habari inayohusiana na hii: Iran: FIFA iipige marufuku Israel kufuatia mapigano Gaza

Rais wa FIFA Gianni Infantino, ameelezea mpango huo wakati wa kongamano la FIFA leo baada ya wawakilishi wa mashirikisho ya soka ya Palestina na Israel kupata fursa ya kuzungumza mbele ya bodi ya shirikisho hilo la FIFA lenye wanachama 211.

Infantino amesema kutoka sasa, FIFA itatumia utaalamu huru wa kisheria kuchambua maombi matatu kutoka Shirikisho la Soka la Palestina FA na kuhakikisha sheria za FIFA zinatumika kwa njia sahihi na kwamba tathmini hiyo ya kisheria itahitajika kuruhusu maoni na madai ya Israel na Palestina.

Matokeo na mapendekezo yatawasilishwa kwa baraza la FIFA.