1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya EU-Mercosur kuanza kutekelezwa kwa muda

27 Februari 2026

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema umoja huo utatekeleza kwa muda makubaliano ya biashara huria kati yake na mataifa manne ya Amerika Kusini.

https://p.dw.com/p/59XY1
Umoja wa Ulaya kuanza kutekeleza kwa muda makubaliano ya kibiashara na Mataifamanne ya Amerika Kusini
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Frederick Florin/AFP/Getty Images

Utekelezaji huo wa muda umetangazwa kuanza licha ya kuwa bado mahakama ya haki inaendelea kuyatathmini.

Tangazo hilo limetolewa Ijumaa baada ya Uruguay na Argentina kuyaidhinisha makubaliano hayo ingawa tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji haijabainishwa. Brazil na Paraguay bado hazijayaidhinisha lakini yanatarajiwa kufanya hivyo hivi karibuni.

Makampuni ya Ulaya, Argentina na Paraguay kuanza kunufaika

Hatua ya Ulaya kuanza kuyatekeleza makubaliano hayo kwa muda inayaruhusu makampuni ya Umoja wa Ulaya, Argentina na Paraguay kunufaika na kanuni mpya za forodha kabla ya makubaliano hayo kuanza kutekelezwa rasmi.

Uamuzi huo hata hivyo umekosolewa vikali na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyeuita wa kushangaza na kuwa kufanya hivyo kabla ya tathmini ya mahakama ya haki ni tabia mbaya na kumeishtusha Ufaransa.