1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chuo kikuu cha pamoja kati ya Ujerumani na Uturuki kufunguliwa

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAGG

BERLIN

Ujerumani na Uturuki zimekubaliana kufungua chuo kikuu cha pamoja mjini Instanbul kufikia mwishoni mwa mwaka ujao wa 2009.Hatua hiyo inalengwa kuimarisha uhusiano wa kitamaduni kati ya nchi hizo mbili. Kiasi cha wanafunzi 5,000 watakaohitimu katika chuo cha pamoja watapata shahada zitakazotambulika na nchi hizo.Mpango huo umetiwa saini hapo jana mjini Berlin na Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir pamoja na mwenzake wa Uturuki Ali Babacan na waziri wa elimu wa Ujerumani Annettte Schavan.