1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

China yataka mauaji ya raia yakomeshwe Ukanda wa Gaza

7 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China Wangi Yi ameitaka Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya raia katika vita vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dFeg
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi
China inasema mzozo kati ya Israel na Hamas unaweza kutatuliwa kupitia suluhisho la mataifa mawili Picha: Wang Zhao/AFP

Yi amesema hakuna sababu ya kuendelea kwa mgogoro huo. "Ni janga la kibinaadamu na fedheha kwamba katika karne hii ya 21, madhila haya ya kibinaadamu hayawezi kukomeshwa. Hakuna sababu ya kuendelea na mgogoro huu, na hakuna kisingizio chochote cha kuendelea kuwauwa raia wasiokuwa na hatia."

Akizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa bunge la Chila, Wang Yi amesema wafungwa wote wanapaswa kuachiwa huru na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono hatua za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Ameongeza kuwa mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas unaweza kusuluhishwa kupitia utekelezwaji kikamilifu wa suluhu ya mataifa mawili na haki ya watu wa palestina. Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa China amesema azma ya Wapalestina ya kuwa dola huru haiwezi tena kuepukika.